
VIGOGO SIMBA WAKOMALIA ISHU YA CHAMA
VIGOGO wa Kamati ya Usajili ya Simba, chini ya Mtendaji Mkuu (C.E.O.) wa timu hiyo, Barbara Gonzalez, wameona isiwe shida na kuchukua maamuzi ya kupanda ndege kumfuata kiungo wao mchezeshaji Mzambia Clatous Chama anayekipiga RS Berkane ya nchini Morocco. Kiungo huyo anawindwa vikali na Yanga katika usajili huu wa dirisha dogo lililofunguliwa Desemba16, mwaka huu kwa ajili ya kukiboresha kikosi hicho. Simba imepanga kukiboresha…