HABARI ZA VURUGU KWENYE MECHI ZISIPEWE KIPAUMBELE KABISA

    HABARI mbaya ambazo nimesikia kutoka kwa ndugu zetu KMC ni kwamba wamepata mateso makubwa kwenye suala la mapokezi walipokuwa kwenye mchezo wao dhidi ya Geita Gold.

    Sina uhakika kama ni hawahawa Geita Gold watakuwa wamefanya hivi ama kuna watu wengine ambao wapo nyuma wakitumia jina la Geita Gold lakini katika hili kwa kweli sijapenda.

    Ndugu yangu Christina Mwagala ambaye ni Ofisa Habari wa KMC ameongea kwa masikitiko makubwa na ameonesha kuwa ile furaha ya awali kuelekea kumenyana na Geita Gold imekwisha kabisa.

    Ambacho kinamshangaza Christina ni namna ambavyo timu ya Geita ambayo ni mali ya Halmashauri ikifanya mambo ya hovyo mbele ya timu ya Halmashauri.

    Lakini hili nalo linafikirisha ujue yaani ndugu kwa ndugu wanafanyiana undugu sasa wengine wakienda huko kama mambo yaspokuwa sawa hali itakuaje?

    Huenda inaweza kuwa mbaya zaidi lakini katika hili ni lazima ukweli uweze kujulikana na kila kitu kiwekwe wazi kama ni kweli ni watu wa Geita Gold wenyewe ama ni watu ambao sio wapenda maendeleo ya mpira wetu.

    Kwa jambo hili ambalo limetokea basi iwe fundisho kwa wengine kwamba mpira sio uadui ila ni burudani na kila mmoja anapata ushindi kutokana na maandalizi ambayo atayafanya.

    Uzuri ni kwamba kila timu inapata dk 90 hivyo iwe ni KMC, Njombe Mji,Lipuli wote hawa dk zao ni hizohizo ile iliyofanya maandalizi mazuri ina uhakika wa kupata ushindi.

    Rai yangu kwa timu zote kwa sasa kuweka mipango sawa hasa katika maandalizi yao uwanjani suala la kuleta mipango ya hovyo nje ya uwanja haifai.

    Ngumu kuamini kwamba kwa sasa kila timu inaweza kushinda mechi zote bila maandalizi hilo ni lazima na muhimu kufanyika.

    Kila mmoja na afanye kazi kwa juhudi katika kutimiza majukumu yake na hili ni muhimu kwa kuwa hakuna ambaye anaamini kwamba anaweza kupata ushindi ikiwa hataweza kujiweka vizuri.

    Wachezaji jukumu lenu kubwa kushirikiana uwanjani wakati wa kusaka matokeo muda huu ni hesabu kukamilisha kwa kuwa hakutakuwa na muda mwingine mpaka msimu ujao.

    Viongozi pia ni wakati wa kuacha amani itawale kwenye maandalizi ya kila mchezo iwe ni ugenini ama nyumbani kila timu inahitaji kupata ushindi.

    Ipo wazi kwamba malengo ya viongozi ni kuona timu inapata ushindi lakini haina maana kwamba kuwepo na matumizi ya nguvu hilo sio sawa kwa afya ya soka letu.

    Bado ligi inaendelea, hakuna timu ambayo imetangazwa kushuka wala kutwaa ubingwa sasa hizo fujo zinatokea wapi kwa wakati huu wa mzunguko wa pili?

    Yale malengo ambayo yalikuwa yamewekwa mzunguko wa kwanza basi lazima yatazamwe na kuendelea kuyafuatilia kwa ukaribu kwani muda bado upo.

    Poleni KMC kwa yalitokea,poleni Geita Gold nina amini kwamba jambo hili litafanyiwa kazi na mamlaka husika ili kuweza kuja na majibu sahihi kwa mechi zijazo.

    @Dizo_Click.

    Previous articleKIUNGO YANGA AINGIA ANGA ZA AZAM FC
    Next articleSIMBA BADO HAWAIFIKIRII MECHI YAO DHIDI YA YANGA