
KMC YASHUSHA PRESHA KWA MASHABIKI WAKE
UONGOZI wa KMC umewataka mashabiki wasiwe na presha juu ya usajili wao kwa kuwa wanajua kile ambacho wanafanya. Kwa sasa KMC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery imekuwa ikiwapukutisha mastaa wake ambao mikataba yao imeisha na wengine kupata madili mapya kwa msimu ujao. Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wanatambua kile ambacho wanakifanya…