Home International RONALDO KUTUA NAPOLI

RONALDO KUTUA NAPOLI

 NYOTA Cristiano Ronaldo anaweza kutua ndani ya Klabu ya Napoli kabla ya usajili kufungwa kesho Septemba Mosi.

Wakala maarufu duniani, Jorge Mendes anapambana kuhakikisha staa huyo anayetaka kuondoka Manchester United anapata changamoto mpya.

Taarifa zimeeleza kuwa dili lake la kujiunga na Napoli litahusisha kubadilisha baadhi ya wachezaji.

Cr 7 mwenye Ballon d’Or tano aliwaambia viongozi wa Manchester United kuwa anataka kuondoka katika timu hiyo ili akashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Imekuwa ngumu kupatikana kwa ofa zake kutokana na gharama ya kumpata staa huyo ambaye mkwanja wake ni mrefu.

Napoli inataka kumchukua Ronaldo akawe mbadala wa Victor Osimhen kama Mnigeria huyo ataondoka kwenye timu hiyo.

Previous articleHUYU NDIYO MSIHINDI WA WIKI, MILIONI 60+ KWENYE KASINO YA MERIDIANBET!
Next articleMASTAA WAWILI SIMBA WAONGEZA NGUVU KUIVAA AL HILAL