WACHEZAJI STARS KAZI IPO KWENU KUJITUMA KUTAFUTA MATOKEO

    IMESHATOKEA kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wachezaji wa ndani, (CHAN) kwa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kupoteza.

    Hamna namna ilikuwa lazima iwe hivyo kwa sababu mpira ni mchezo wa makosa na pale ambapo wachezaji walikosea wapinzani wakatumia nafasi hiyo kuweza kutuadhabi.

    Matokeo huwezi kubadili itakuwa hivyo vizazi na vizazi vitajua kwamba Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Uganda Uwanja wa Mkapa.

    Tumeona baada ya hayo kutokea benchi la ufundi limeweza kufanyiwa mabadiliko na Kim Poulsen ambaye alikuwa anaongoza timu akiwa ni kocha mkuu amevuliwa mamlaka na kurejeshwa kwenye timu za Taifa za Vijana.

    Sawa ameondoka Kim je wachezaji na mbinu zitabadilika kwa ajili ya kuwakabili Uganda kwenye mchezo ujao wa marudio.

    Kuna mpango mwingine wa kuweza kuboresha viwango vya wachezaji kwa mechi zijazo na zile ambazo wachezaji wanaocheza leo watakuwa wametundika daruga?

    Umuhimu kwa sasa ni mkubwa kufanya uwekezaji kwa vijana na kuwekeza nguvu kubwa kwenye ligi hizi za madaraja ya chini ambayo yana vipaji vingi na vikubwa.

    Wachezaji wa ndani wamekuwa wakicheza mechi zao katika hali ile waliyoizoea na kusahau kwamba wanapambania taifa wanapaswa kujitoa kwa hali na mali.

    Muhimu wakati huu wa mpito wa benchi la ufundi kwenye timu ya taifa na kwa wachezaji pia upite ule mpito wa kujitoa kwa kuogopa na kuingia kwenye hali ya kujitoa kwa kujituma muda wote.

    Walianza kwa kusuasua kwenye mechi dhidi ya Somalia tukaongea kwamba wanapaswa kuongeza juhudi kwa kuwa kila hatua ni ngumu imekuwa hivyo kazi bado haijaisha kwao

    Kete ya mwanzo ilianza kuchezwa wakiwa nyumbani licha ya kwamba Somalia wao walikuwa wenyeji na ilionekana namna gani waliweza kuanza kazi kwenye mchezo huo wa kwanza.

    Mashabiki walijitokeza kuweza kuona burudani kwenye mchezo huo na matarajio yao illikuwa ni kwenye kupata ushindi kwa timu ya Taifa.

    Ilikuwa ngumu licha ya kupata ushindi wa bao 1-0 hivyo mchezo ujao ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa hapo lazima wachezaji waweze kulipa deni na kukata kiu kwa mashabiki.

    Kazi bado inaendelea wachezaji mna deni kuweza kufanya vizuri kwa mechi ijayo ya marudio kwani ushindi wa jumla ya mabao 3-1 mliopata dhidi ya Somalia lazima uonekane kwenye hatua hii ya muhimu.

    Septemba 3 ipo njiani na mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa namna yoyote katika mchezo huo tuna amini kwamba wachezaji mnaweza kupata matokeo.

    Umakini wa wachezaji na kufanya kila kitu kwa kujituma na kufuata malekezo ya benchi la ufundi ni muhimu kuweza kwenda sawa na kasi ambayo ipo.

    Jukumu lenu wachezaji kwa sasa na kwa mechi zijazo ni kujituma na kufanya kazi kwa umakini zaidi ya mechi iliyopita na makosa yapo lakini lazimayapungue na umakini uongezeke.

    Tayari Kaimu Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” Honour Janza ameanza kazi kuinoa Stars kuelekea mchezo dhidi ya Uganda unaotarajiwa kuchezwa Septemba 3,2022.

    Previous articleKIUNGO WA KAZI SIMBA AINGIA KWENYE VITA
    Next articleWAMEANZA MSIMU KWA MAJANGA MASTAA HAWA