Cape Verde na Curaçao Waingia Kwenye Historia ya Kombe la Dunia la FIFA 2026

Curacao's players pose for a team photo before the start of the World Cup qualifier football match between Jamaica and Curacao at the National Stadium in Kingston, Jamaica on November 18, 2025. (Photo by Ricardo Makyn / AFP) (Photo by RICARDO MAKYN/AFP via Getty Images)

Kombe la Dunia la FIFA 2026 linatarajiwa kuandika historia mpya huku mataifa kadhaa yakirejea baada ya miongo mingi na mengine yakifuzu kwa mara ya kwanza kabisa kwenye mashindano hayo makubwa ya soka duniani.

Mashindano hayo yatakayofanyika kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, 2026 yatakuwa na muundo mpya uliopanuliwa, jambo lililofungua nafasi kwa timu nyingi zaidi kushiriki na kuandika simulizi mpya katika dunia ya soka.

Miongoni mwa mataifa yaliyoandika historia ni Cape Verde, ambayo imefuzu kwa mara ya kwanza licha ya kuwa na idadi ndogo ya watu wasiopungua laki sita. Mafanikio yao yamechagizwa na nidhamu kubwa pamoja na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa Ulaya.

Pia Curaçao imeweka rekodi ya kuwa taifa lenye idadi ndogo zaidi ya watu kuwahi kufuzu Kombe la Dunia, ikiwa na wakazi takribani 150,000 pekee.

Kwa upande mwingine, Jordan imefanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza baada ya karibu miaka 40 ya majaribio, huku Uzbekistan nayo ikiweka historia kama taifa la kwanza kutoka Asia ya Kati kufuzu Kombe la Dunia.

Aidha, Democratic Republic of the Congo na Haiti zinarejea kwenye michuano hiyo baada ya miaka 52 tangu kushiriki kwa mara ya mwisho mwaka 1974, huku Iraq ikirejea tena baada ya miaka 40 tangu iliposhiriki mwaka 1986.