Yanga SC yamfuta kazi Kocha Mkuu Pedro Goncalves

Klabu ya Yanga imemfuta kazi kocha Pedro Goncalves leo Mei 6, 2026 muda mfupi baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya KMC FC, Uwanja wa KMC Complex.

Goli la ushindi kwenye mchezo wa leo limefungwa na Allen Okello dakika ya 65 limedumu mpaka mwisho wa mchezo huku kiungo huyo akichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Taarifa iliyotolewa leo na uongozi wa klabu hiyo haijaweka wazi sababu za uamuzi huo, ila imetaja ambao watakinoa kikosi hicho kwenye mechi ambazo zimebaki.

“Kikosi chetu kitakuwa chini ya uongozi wa Kocha Abdihamid Moalin pamoja na Kocha Patrick Mabedi hadi mwisho wa msimu,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.