KMC FC vs Yanga SC ni ratiba inayofuata ndani ya NBC Premier League leo Mei 6, 2026 Uwanja wa KMC Complex.
KMC FC imecheza mchezo mmoja na mabingwa watetezi katika msimu huu na ilipoteza kwa kufungwa magoli 4-1 hivyo leo ni mchezo wa mzunguko wa pili.
Pedro Goncalves, Kocha Mkuu wa Yanga SC amesema kuwa wanachohitaji ni alama tatu kwenye kila mchezo ikiwemo leo dhidi ya KMC FC iliyo nafasi ya mwisho kwenye msimamo na pointi 9.
Yanga SC inaongoza ligi ikiwa na pointi 48 mchezo uliopita iligawana pointi mojamoja na Simba SC kwa kufungana magoli 2-2.
Pedro amesema: “Haijalishi tunacheza na nani, lengo letu ni kukusanya alama tatu kwenye kila mchezo, hivyo tutakuwa makini kwenye mchezo wetu muhimu.
“Ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuhakikisha kwamba tunawaheshimu KMC huku tukiingia na malengo yetu ya kushinda mchezo. Kikubwa ni kupata pointi baada ya mchezo,”.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.