KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ni kinara wa utupiaji magoli ndani ya BC Premier League.
Katika mchezo wa Mei 5, 2026 uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 1-0 Namungo FC.
Goli la ushindi limefungwa na Feisal dakika ya 41 kwa mkwaju wa penati. Hivyo anafikisha magoli 10 ndani ya ligi 2025/26 akiwa namba moja kwenye chati ya wafungaji.
Kwa mujibu wa rekodi Ligi Kuu Tanzania Bara kiungo huyo alikuwa na magoli 9 sawa na Prince Dube wa Yanga SC hivyo kufunga kwake goli moja ameongeza idadi akiwa namba moja kwa sasa.
Azam FC imecheza jumla ya mechi 21 haijapoteza mchezo kwenye msimamo ipo nafasi ya pili na pointi 43.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.