Kombe la Muungano leo Jumatano Aprili 22, 2026 linaendelea ikiwa ni hatua ya robo fainali kwa wababe wawili kushuka uwanjani kusaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali.
Uwanja wa New Amaan saa 1:15 usiku utapigwa mchezo mmoja utakaowakutanisha KVZ vs AzamFC.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge amesema wapo tayari kwa mchezo huo malengo ni kupata ushindi.
Aprili 21, 2026 ulichezwa mchezo wa ufunguzi katika hatua ya robo fainali ilikuwa Yanga SC vs Muembe Makuti.
Mabingwa watetezi Yanga SC wamekata tiketi kutinga hatua ya nusu fainali Muungano Cup 2026.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.