Senegal yaichapa Sudan 3-1 yatinga robo fainali AFCON 2025

TIMU ya Taifa ya Senegal imekata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali AFCON 2025, Morocco. Timu hiyo ilianza kufungwa napema kipindi cha kwanza dhidi ya Sudan. Kabla hawajaenda mapumziko waliweka usawa na kuongeza goli moja.

Senegal 3-1 Sudan mchezo wa hatua ya 16 bora umegota mwisho. Ni Aamir Abdallah alipachika goli la kuongoza kwa Sudan. Dakika ya 29 Senegal walisawazisha na kuongeza goli la pili dakika ya 45+3 kupitia kwa Pape Gueye. Goli la tatu ni kipindi cha pili limefungwa na Ibrahim Mbaye dakika ya 77.

Mchezo huo umechezwa Grand Stade de Tanger ulikuwa na ushindani mkubwa. Senegal walipiga jumla ya kona 7 huku Sudan wakipiga kona 4 pekee kwenye mchezo ndani ya dakika 90.

Kesho Januari 4,2026 timu ya taifa ya Tanzania itakuwa kwenye kazi kusaka tiketi kutinga hatua ya robo fainali itakuwa dhidi ya Morocco ambao ni wenyeji.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.