SALAH ATAJA HATMA YAKE LIVERPOOL

MOHAMED Salah mshambuliaji namba moja kwa kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu England akiwa ametupia mabao 16 amesema kuwa hatma yake kubaki ndani ya kikosi cha Liverpool ipo mikononi mwa bodi ya klabu hiyo.

Suala la Salah kusaini mkataba mpya ndani ya Liverpool limekuwa likizungumzwa tangu mwaka jana 2021 ila mpaka sasa hakuna muafaka uliofikiwa.

Salah anatarajiwa kumaliza mkataba wake ndani ya miezi 18 ijayo katika klabu yake na yeye anatamani kustaafu akiwa kwenye timu hiyo.

Alitua Liverpool 2017 akitokea kikosi cha Roma kwa pauni milioni 34.