IMEELEZWA kuwa Clatous Chama na Simba tayari wamemalizana kila kitu kuhusu usajili wake na kilichobaki ni kutambulishwa.
Chama kwa sasa ni mali ya RS Berkane ambapo aliibuka huko msimu wa 2021/22 akitokea Klabu ya Simba.
Moja ya usajili ambao umekuwa na mvutano mkubwa ni wa Chama kwa kuwa wakati Simba wakipambana kuinasa saini yake na Yanga pia wanatajwa kuiwinda saini hiyo.
Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa bado dirisha la usajili halijafungwa hivyo chochote kinaweza kutokea.
“Bado usajili unaendelea na usajili wa Tanzania ni tofauti na Ulaya ambao huwa wanaweka mambo wazi, tusubiri bado dirisha halijafungwa,”.
Dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa Januari 15 na lilifunguliwa Desemba 16,2021 na mpaka sasa Simba bado haijatambulisha mchezaji.