NYOTA Ismail Mhesa rasmi ametambulishwa ndani ya Mtibwa Sugar kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Januari 12,2022 alitambulishwa katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Salum Mayanga ambaye alikuwa akikinoa kikosi cha Tanzania Prisons.
Mhesa alikuwa ndani ya Mtibwa Sugar msimu wa 2020/21 lakini msimi wa 2021/22 hakuanza maisha ya soka la ushindani na Mtibwa Sugar ambao walianza msimu wakinolewa na Joseph Omong ambaye alichimbishwa.
Mtibwa Sugar imecheza jumla ya mechi 11 ipo nafasi ya 13 na ina pointi 10 kibindoni.