Home Sports AZAM FC:TUTAFUNGA MPAKA SHULE,YANGA TUMEWAFUNGA SANA

AZAM FC:TUTAFUNGA MPAKA SHULE,YANGA TUMEWAFUNGA SANA

ZAKARIA Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC a,ewela wazi kuwa baada ya kuifunga Yanga sasa wanaamini kwamba watafunga mpaka shule hadi Ramadhan.

Kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa Uwanja wa Amman, Azam FC iliwaondoa Yanga ambao walikuwa ni mabingwa watetezi kwa penalti 9-8 baada ya dakika 90 kutoshana nguvu bila kufungana.

Sasa leo Januari 13, saa 2:15 usiku Azam FC itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchez wa fainali dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Amaan.

Thabit amesema:”Nashangaa watu wengi wamekuwa wakitupongeza baada ya kuifunga Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi lakini ukweli ni kwamba huwa tunaifunga sana Yanga tukikutana nayo kwenye Kombe la Mapinduzi.

“Baada ya kuifunga Yanga sasa tutafunga mpaka shule na tunakwenda kufunga mpaka Ramadhan, kikubwa ni kwamba tunajiamini na tunataka kwenda kufanya jambo kubwa.

“Kuhusu ubingwa ipo wazi kwamba sisi ni mabingwa wa kihistoria na tunalihitaji Kombe la Mapinduzi tutafunga tu kila kitu mwaka huu tunafungafunga tu sisi tupo vizuri,” amesema.

Azam na Simba zimekutana mara tatu kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi na ni Azam FC ilisepa na taji hilo mara zote

Ilikuwa ni 2012,2017 na 2019 hivyo leo Januari 13,2022 inakuwa ni mara ya nne kwa wababe hawa kukutana uwanjani.

Previous articleMHESA ATAMBULISHWA MTIBWA SUGAR
Next articleSIMBA:TUNALITAKA KOMBE LA MAPINDUZI