Home International MWAMUZI HUYU AFCON ALITIBUA KWELI MAMBO

MWAMUZI HUYU AFCON ALITIBUA KWELI MAMBO

MWAMUZI kutoka nchini, Zambia Janny Sikazwe amezua gumzo kwenye michuano ya AFCON inayoendelea kutimua vumbi huko Cameroon wakati wa mchezo wa kundi F kati ya Tunisia na Mali uliomalizika kwa Mali kuibuka na ushindi wa 1-0.

Maamuzi ya utata yaliyotolewa na refa huyo katika mchezo huo yamezua mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii na kuzua sintofahamu ya utimamu wa mwamuzi huyo kiafya hususani katika kipindi cha pili cha mchezo huyo.

Refa Janny awali alipuliza kimakosa kipyenga cha kumaliza mtanange huo dakika ya 85 tu kabla ya kupata shinikizo kutoka kwa wachezaji na Benchi la ufundi la Tunisia na kubatilisha uamuzi huo.

Hata hivyo mara tu baada ya kuruhusu mchezo kuendelea refa huyo akamuonesha kadi nyekundu iliyokuwa na utata mkubwa mshambuliaji wa Mali El Bilal Toure kabla ya kuibua utata mwingine kwa kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo huo dakika ya 89 bila ya kuwa na sababu maalumu kitendo kilichowakera Tunisia.

Novemba 20,2018 CAF iliwahi kumfungia refa huyo baada ya kubainika kupokea rushwa na kuharibu mchezo wa nusu fainali ya pili wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya Espérance de Tunis ya Tunisia walioshinda 4–2 dhidi ya Primeiro de Agosto.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI
Next articleSALAH ATAJA HATMA YAKE LIVERPOOL