Azam FC vs Singida Black Stars wakubwa kazini

DESEMBA 3,2025 Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea ambapo wakubwa wawili watakuwa kazini katika msako wa pointi tatu muhimu.

Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Florent Ibenge vs Singida Black Stars chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi mbinu zao zitakuwa zinapambana.

Hii ni ligi namba nne kwa ubora Afrika imekuwa na ushindani mkubwa huku mabingwa watetezi wakiwa ni Yanga SC ambao wao mchezo wao ujao ni dhidi ya Fountain Gate.

Azam FC vs Singida Black Stars ngoma inatarajiwa kuchezwa saa 3:00 usiku huku miongoni mwa wachezaji walio tayari ni Feisal Salum kwa Azam FC na Khalid Aucho wa Singida Black Stars hawa wote waliwahi kucheza Yanga SC.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.