Kagera Sugar 0-2 Simba SC, NBC Premier League

UBAO wa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba baada ya dakika 90 umesoma Kagera Sugar 0-2 Simba SC, NBC Premier League.

Mabao ya ushindi kwa Simba SC yamefungwa na Ismail Toure dakika ya 45 kwa pigo la kichwa na Ellie Mpanzu dakika ya 69 kwa pigo la mguu wa kulia.

Mtengeneza asisti za mabao yote mawili ya ushindi kwa kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Steve Berkar ni Lbase Gueye ambaye amekuwa kwenye ubora ndani ya dakika 90.

Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Ibrahim Doumbia ni miongoni mwa walioanza kikosi cha kwanza na alifanya jaribio ambalo liligonga mwamba dakika ya 4 kipindi cha kwanza cha mchezo.

Matokeo haya yanaifanya Simba SC kuanza kwa ushindi mchezo wa kwanza ugenini wakishinda dhidi ya Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Kaseja.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Duniani kote kinapatikana mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.