RALF AKIRI NYOTA MAN U WANATAKA KUSEPA

RALF Rangnick, Kocha Mkuu wa Manchester United kwa muda amekiri kwamba mastaa kadhaa wa timu hiyo wanataka kuondoka mara tu baada ya mikataba yao kuisha.

Hivi karibuni ilielezwa kuwa mastaa 17 wa kikosi cha Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu England wanataka kuondoka kutokana na kuona mambo hayaendi ndani ya timu hiyo.

Kocha huyo hajaweka wazi wachezaji ambao wanataka kuondoka katika kikosi hicho isipokuwa Anthony Martial ambaye aliweka wazi kwamba anataka kuondoka.

Wachezaji wengine ambao wanatajwa kwamba wanaweza kuondoka ni pamoja na Paul Pogba,Jesse Lingard, Edson Canvan na Juan Mata ambapo baadhi yao mikataba yao inatarajiwa kuisha.

Kocha huyo amesema:”Tuna wachezaji ambao mikataba inamalizika mwishoni mwa msimu lakini tuna wachezaji wawili watatu wenye mikataba ambao wanataka kuondoka,”.

Kocha huyo mpaka sasa  amekaa benchi kwenye mechi sita na ameshinda mechi tatu kupoteza moja na kuambulia sare mechi mbili.