Home International VAR KUTUMIKA AFCON, MAMBO YANAANZA LEO

VAR KUTUMIKA AFCON, MAMBO YANAANZA LEO

HATIMAYE kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano ya AFCON, mechi zote 52 zitatumia marefa wasaidizi wa picha za video (Video Assistant Referees – VAR) huko Cameroon.

Michuano hiyo itaanza rasmi leo Jumapili Januari 9, 2022 ambapo wenyeji Cameroon watacheza na Burkinafaso katika uwanja wa Olembe huko Yaounde. Mechi ya mwisho itachezwa Februari 6 katika uwanja huohuo.

Wafanyakazi 63 watakuwepo wakijumuisha marefa 24, marefa wasaidizi 31 na marefa wasaidizi wa picha za video (VAR) 8.

Katika marefa hao wanawake ni wanne, Salima Mukasanga (Rwanda), Carine Atemzabong (Cameroon), Fatiha Jermoumi (Morocco) na Bourcha Karboubi (Morocco).

Previous articleRALF AKIRI NYOTA MAN U WANATAKA KUSEPA
Next articleVIDEO:POPAT AZUNGUMZIA MCHEZO WAO DHIDI YA YANGA