Orodha ya makipa wenye clean sheet nyingi NBC Premier League

VITA ya NBC Premier League kwenye eneo la makipa kutoka na clean sheet baada ya dakika 90 inazidi kushika kasi msimu wa 2026/27. Djibrilla Kassali wa Simba SC amekusanya hati safi 4 sawa na Djigui Diarra wa Yanga SC.

Mussa Mbisa wa Dodoma Jiji anazo hati safi 3 sawa na Christopher Nyakanda wa Polisi Tanzania,Toba Kutisha wa Mbeya City na Suleiman Abraham wa Namungo FC.

Diarra mchezo pekee ambao alifungwa mabao mengi ulikuwa wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Oktoba 10,2026.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 2-1 Yanga SC, mabao yalifungwa na Neo Maema dakika ya 68 na Ellie Mpanzu dakika ya 71 kwa upande wa Yanga SC mtupiaji alikuwa ni Peter Shalulile dakika ya 5.

Simba SC ambao ni vinara wamecheza mechi 8 wamekusanya pointi 24 huku Yanga SC ikiwa imecheza mechi 7 imekusanya pointi 18.

…

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar

Moyo Wangu Unavuja Damu: https://selar.com/7901h4koj4