Mechi zote za Simba SC CAF kupigwa Uwanja wa Uhuru

UONGOZI wa Simba SC umebainisha kuwa mechi zote mbili CAF Champions League dhidi ya de Agosto zitachezwa Dar, Uwanja wa Uhuru.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema maandalizi yanaendelea kuelekea mechi zijazo za kimataifa na wapo tayari kusaka matokeo chanya.

“Kuelekea mechi zetu za Ligi ya Mabingwa Afrika 20/10/2026 tutakuwa uwanjani saa 10:00 jioni, Simba SC watakuwa wageni mkondo wa kwanza, Uwanja wa Uhuru.

“25/10/2026 Simba SC saa 10:00 jioni hapa tutakuwa wenyeji kwenye mchezo wetu Uwanja wa Uhuru kusaka ushindi.Mazungumzo ya awali wapinzani de Agosto waligusia mechi ya kwanza haitakuwa na mashabiki wao watakuwa wenyeji.Mechi ya pili ya marudioano ambayo Simba SC tutakuwa wenyeji itakuwa na mashabiki,” amesema Ahmed.

…

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar

Moyo Wangu Unavuja Damu: https://selar.com/7901h4koj4