Lamine Yamal ameendelea kuonyesha kiwango bora baada ya kuhusika moja kwa moja katika mabao matatu wakati Hispania ikiichapa Croatia kwa mabao 4-1 katika mchezo wa UEFA Nations League.
Yamal alianza kwa kufungua akaunti dakika ya pili, kabla ya Marc Pubill kuongeza bao la pili dakika ya 31.
Croatia ilifanikiwa kupata bao la kufutia machozi kupitia Dion Drena Beljo dakika ya 28, lakini Hispania iliendelea kutawala mchezo.
Kipindi cha pili, Yamal alifunga bao lake la pili dakika ya 63 na kukamilisha brace, kabla ya Nico Williams kufunga bao la nne dakika ya 89 na kuhitimisha ushindi wa Hispania wa mabao 4-1.
Mbali na kufunga mabao mawili, Yamal pia alitoa assist kwa bao la Pubill, hivyo kuhusika moja kwa moja katika mabao matatu ya Hispania.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotajwa, Yamal amefikisha jumla ya michango 18 ya mabao (G/A) katika michezo yake nane iliyopita. Katika michezo miwili ya hivi karibuni akiwa na timu ya taifa ya Hispania, amehusika na mabao mawili pamoja na assist moja.