CR7 Hajastaafu! Ronaldo Aitwa Kwenye Kikosi Cha Kwanza Cha Jorge Jesus

Cristiano Ronaldo ataendelea kuitumikia timu ya taifa ya Portugal baada ya kutajwa kwenye kikosi cha kwanza cha kocha mpya, Jorge Jesus, kwa ajili ya michezo ijayo ya UEFA Nations League.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 41, ameendelea kuwa sehemu ya mipango ya Portugal licha ya awali kueleza kuwa Kombe la Dunia la 2026 lilikuwa la mwisho kwake kushiriki. Kuitwa kwake kunamaanisha bado ataendelea kuonekana kwenye kikosi cha taifa katika kipindi hiki kipya chini ya Jorge Jesus.

Jorge Jesus, ambaye hapo awali aliwahi kuwa kocha wa Ronaldo katika klabu ya Al-Nassr, ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya kuanza kampeni ya Nations League. Ronaldo yupo pamoja na nyota wengine akiwemo Bruno Fernandes, Bernardo Silva, Rafael Leao, Joao Felix na Vitinha.

Portugal itaanza michezo yake dhidi ya Wales Septemba 24, kabla ya kusafiri kucheza na Norway Septemba 27. Baadaye itakutana na Denmark Oktoba 1 na Norway tena Oktoba 4.

Ronaldo pia anaendelea kusaka kufikisha jumla ya mabao 1,000 katika career yake, akiwa amebakiza mabao 21 kufikia hatua hiyo, kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni.