Simba SC vs 15 De Agosto ya Guinea ya Ikweta CAF Champions League

SIMBA inatarajiwa kuvaana dhidi ya 15 De Agosto ya Guinea ya Ikweta(Equatorial Guinea) katika hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa kusaka hatua ya mtoano ili kusaka tiketi ya kuingia makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo hwa kwanza utachezwa kati ya Oktoba tarehe 17 -18, 2026 huku Simba ikitakiwa kuanzia ugenini

Na mchezo wa pili utachezwa kati ya 24 au 25 Oktoba, Simba ikiwa nyumbani, 15 De Agosto ni Mabingwa wa Ligi Kuu ya Guinea ya Ikweta msimu uliopita.

Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker ilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa jumla ya mabao 7-1 dhidi ya Mighty Wanderers uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Septemba 13, 2026.

Ni rekodi ya ushindi mkubwa ambao timu hiyo imepata ikiwa nyumbani na imeshinda nje ndani katika dakika 180.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar