Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi amesema wanatambua wana mchezo mgumu vs Geita Gold ambao watakutana nao leo Septemba 15, 2026 kwenye mchezo wa ligi.

Wababe hawa wawili watakuwa na kasi kusaka pointi 3 muhimu Uwanja wa KMC Complex saa 1:00 usiku. Kocha Manqoba amebainisha kuwa anatambua mbinu wanazotumia wapinzani wao katika kusaka ushindi.

“Tunakwenda kukutana na timu nzuri. Ina wachezaji wenye uwezo mkubwa kiufundi ni timu yenye mpangilio mzuri, iliyoshikamana kwenye ulinzi na yenye uwezo mkubwa wa kufanya mashambulizi ya kushtukiza. Ni timu ambayo inaweza kushangaza na kuifunga timu yoyote, hivyo tunafahamu hatuchezi dhidi ya wapinzani wepesi.

“Sina presha, niko kwenye nafasi ambayo nilitamani kuwa. Tunapaswa kufurahia ushindani na kuona mapambano yataishia wapi. Hii ni ligi yenye ushindani mkubwa na bado hatujacheza dhidi ya baadhi ya timu kubwa, hivyo tunapaswa kuchukua mchezo mmoja baada ya mwingine,” .

Yanga SC kwenye msimamo wa ligi inaongoza ikiwa na pointi 15 baada mechi 5 inakutana na Geita Gold iliyo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 7 kibindoni.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar