NYOTA wawili wa kikosi cha Yanga SC, nahodha msaidizi Dickson Job na mshambuliaji Clement Mzize watakosekana kwenye mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ya Botswana.
Sababu kubwa ya wachezaji hao kukosekana ni kutokuwa fiti licha ya kuwa kwenye msafara wa kikosi cha wachezaji 30 waliokwea pipa mapema Septemba 2, 2026.
Kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano Yanga SC, Ali Kamwe, amesema kuwa wachezaji hao wapo kwenye msafara lakini hawatakuwa sehemu ya mchezo.
“Msafara una wachezaji 30 na miongoni mwa hao ni Dickson Job na Clement Mzize lakini hawa hawatakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Gaborone United kwa sababu wataishia Afrika Kusini.
“Wachezaji hawa wanakwenda Medical Checkup zaidi ili kupata taarifa kabla hawajarejea uwanjani, hatutaki kubahatisha kwenye masuala ya wachezaji kurudi uwanjani,”.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.