Mchezo wa raundi ya nne ya Championship utachezwa leo Jumatano, Septemba 2, 2026, saa 21:45 usiku, katika uwanja wa Loftus Road, jijini London. QPR watakuwa wenyeji wakijaribu kuendeleza mwanzo mzuri wa msimu wao mbele ya Cardiff City, timu inayorejea Championship baada ya kupanda daraja msimu uliopita.
Klabu ya QPR ilimaliza msimu uliopita katika nafasi ya kumi na tano ikiwa na alama 58, lakini imeanza msimu huu wa 2026/27 kwa nguvu zaidi. Walianza kwa ushindi wa ugenini dhidi ya Portsmouth, kisha wakatoka sare bila mabao dhidi ya Bolton nyumbani, na hivi karibuni wakaishinda Blackburn Rovers ugenini kwa bao 2-1.
Hata hivyo, walitolewa katika EFL Cup na Millwall kupitia mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1. Changamoto kubwa kwa kocha wa QPR ni orodha ndefu ya majeruhi Boy Kemper, Tariq Lamptey, Justin Obikwu na Karamoko Dembélé wote hawapo kutokana na majeraha, jambo linaloweza kuathiri upangaji wa kikosi.
Timu ya Cardiff ilishuka daraja hadi League One mwaka 2025, lakini ilirejea mara moja baada ya kumaliza msimu katika nafasi ya pili. Kuanzia kwao katika Championship msimu huu kumejaa sare 1-1 dhidi ya Wrexham, na sare mbili za 2-2 dhidi ya Derby County na Sheffield United, ikionyesha timu inayojenga msingi wa ulinzi lakini bado inatafuta ushindi wa kwanza wa msimu. Katika EFL Cup walifanikiwa kuiondoa Swindon Town kwa bao 3-2 kabla ya kutolewa na Norwich City katika raundi iliyofuata.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
QPR wamekuwa na ubora mkubwa dhidi ya Cardiff, wakiwa wameshinda mara 11 dhidi ya ushindi 4 wa Cardiff katika miaka ya hivi karibuni, huku mechi 5 zikiisha kwa sare. Rekodi ya muda mrefu zaidi kati ya vilabu hivi pia inaonyesha QPR wakiwa na ushindi zaidi.
Ukiangalia mwenendo wa sasa QPR wakiwa na ushindi mzuri wa hivi karibuni na faida ya kucheza nyumbani, dhidi ya Cardiff ambao bado hawajapata ushindi wowote kwenye ligi msimu huu QPR wananafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana ubora wao.
Hata hivyo, uwezo wa Cardiff wa kutoka sare mara kwa mara (kama walivyofanya dhidi ya Derbycountry na Sheffield United) unaonyesha timu yenye nidhamu ya ulinzi ambayo inaweza kuwapa QPR wakati mgumu.