Azam FC vs Simba SC kupigwa Septemba 16, 2026

Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC raundi ya 6 kati ya Azam FC vs Simba SC uliopangwa kuchezwa Septemba 9, 2026, umesogezwa mbele hadi Septemba 16, 2026, kupisha maandalizi ya Simba SC kwenye mashindano ya kimataifa ya CAF.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB imefanya mabadiliko hayo kufuatia maombi maalum kutoka kwa uongozi wa Simba SC. Klabu hiyo iliomba kupatiwa muda wa kutosha kujiandaa na mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAF dhidi ya Mighty Wanderers.

Simba SC itacheza mechi mbili muhimu dhidi ya Mighty Wanderers kabla ya kuvaana na matajiri wa Dar kwenye mchezo wa ligi.

Ni Septemba 6, 2026 mnyama atakuwa ugeninidi kukabiliana na Mighty Wanderers ya Malawi.

Na Septemba 13, 2026 itakuwa Simba SC vs Mighty Wanderers mnyama akiwa nyumbani kwenye mchezo wa pili hatua ya awali.

Kete ijayo itakuwa Septemba 16, 2026 Azam FC vs Simba SC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Duniani kote kinapatikana mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.