Mwanza: Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameanza msimu wa NBC Premier League kwa kasi baada ya kuichapa Pamba Jiji FC mabao 2-1 na kuchukua alama zote tatu.
Simba ilipata mabao yake kupitia Clatous Chama dakika ya 18 na Oura dakika ya 30, kabla ya Pamba Jiji kujibu kupitia Diomande dakika ya 72.
Mchezo huo ulikuwa na changamoto kubwa kwa Simba baada ya kiungo Ibraheem Jabaar kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 44, hivyo Wekundu wa Msimbazi kucheza kipindi cha pili wakiwa pungufu.
Licha ya kuwa pungufu kwa zaidi ya dakika 45, Simba ilifanikiwa kulinda ushindi huo hadi filimbi ya mwisho na kujihakikishia alama zote tatu.
Matokeo hayo yanaifanya Simba SC kufikisha alama sita baada ya kucheza mechi mbili katika msimu wa 2026/27 na kupanda hadi kileleni mwa msimamo wa ligi.
FT: Pamba Jiji FC 1-2 Simba SC
⚽ 18’ Chama — Simba
⚽ 30’ Oura — Simba
🟥 44’ Ibraheem Jabaar — Simba
⚽ 72’ Diomande — Pamba Jiji