Usiku wa kuamkia leo, mambo hayakwenda vizuri kwa bondia Hassan Mwakinyo aliyekuwa akiipeperusha bendera ya Tanzania, Abidjan, Ivory Coast kwa kuzipiga na bondia Michel Soro mwenye uraia pacha wa Ivory Coast na Ufaransa.
Mwakinyo alipoteza kwa TKO katika raundi ya tisa kwenye pambano la uzito wa Middleweight la raundi 12 na kushindwa kubeba mkanda wa IBO aliokuwa akiuwania.
Matokeo hayo yamewaibua mashabiki wengi wa ngumi mitandaoni, wanaotoa maoni tofauti tofauti.
Wengi wanampa moyo Mwakinyo na kumtaka asikate tamaa kwa sababu kwenye boxing, siku zote kuna ‘next time’ na kumtaka aongeze kupiga tizi kujiandaa kwa pambano lingine lolote litakalokuja mbele yake ingawa pia wapo wanaoponda.