Coastal Union vs Simba SC kazi inaendelea

Coastal Union vs Simba SC ni mchezo unaofuata kwenye ligi Mei 21, 2025 kwa wababe hawa kusaka pointi tatu muhimu uwanjani.

Huu utakuwa mchezo wa mzunguko wa pili, walipokutana mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo ulisoma, Simba SC 2-0 Coastal Union.

Coastal Union kwenye msimamo ipo nafasi ya 12 ina pointi 25 wapo kambini, Tanga, Uwanja wa Mkwakwani kwa maandalizi kuwakabili wapinzani wao.

Simba SC watakuwa ugenini mchezo ujao wapo nafasi ya pili tayari wametia kambi, Tanga kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo.

Rajab Shamte, Meneja wa Coastal Union amesema wanatambua umuhimu wa mchezo ujao wakiwa nyumbani watapambana kupata pointi tatu muhimu.

“Tunafanya maandalizi kuelekea mchezo wetu muhimu ujao dhidi ya Simba SC, tupo tayari kuwakabili ukizingatia tutakuwa nyumbani,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.