Fainali ya FA CUP inaenda kutimua vumbi wiekndi hii siku ya Jumamosi katika dimba la Wembley huku hili likiwa ni Kombe la heshima kwa timu hizi mbili Chelsea vs Man City pale Uingereza.
Hii ni mechi ambayo inaenda kuwa ya moto zaidi kwani hili ni moja ya pambano la kihistoria ambalo linaenda kutokea kutokana mbinu na presha za sio tu mashbaiki bali wachezaji kwani kila timu inahitaji kuweka heshima katika uwanja huo.
Pep Guardiola na vijana wake, huu ni mchezo wa kulinda hadhi yao baada ya msimu wenye changamoto tofauti na ilivyozoeleka. Kwa miaka mingi City wamekuwa timu inayotawala Uingereza kwa ubora wa kumiliki mpira kwa kiwango cha juu, pressing kali na consistency ya kushinda mataji.
Lakini msimu huu wameonekana kuyumba katika baadhi ya mechi kubwa, jambo ambalo limewafanya wengi waanze kujiuliza kama zama zao za domination zinaanza kupungua. Ndiyo maana FA Cup imekuwa muhimu sana kwao. Kushinda kombe hili kutawapa nafasi ya kumaliza msimu kwa heshima na kuonyesha kuwa bado wao ni timu bora zaidi Uingereza.
Tengeneza pesa leo kwenye michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile Keno, Aviator, Poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Huku kwa Chelsea, huu ni huenda ukawa ni mchezo ambao unaweza kubadilisha kabisa taswira ya klabu yao baada ya miaka kadhaa ya misukosuko, kubadilisha makocha mara kwa mara na kutumia fedha nyingi kwenye usajili bila mafanikio makubwa, Chelsea wanaanza kuonyesha dalili za kujenga timu mpya yenye ushindani.
Wachezaji vijana wameanza kuonyesha ukomavu mkubwa, na mashabiki wanaanza kupata matumaini tena kwamba timu yao inaweza kurejea kwenye ubora wa zamani. Hivyo, kushinda FA Cup dhidi ya Manchester City kutakuwa kama ujumbe rasmi kwamba Chelsea wameanza kurudi kwenye kiwango cha timu kubwa. Suka jamvi hapa.
Takwimu zinaonesha kuwa timu hizi mbili zimekutana zaidi ya mara 180 katika mashindano yote, huku Chelsea wakiwa na ushindi 71 na City ushindi 68. Lakini kinachoumiza mashabiki wa Chelsea ni rekodi ya miaka ya karibuni. Machaguo zaidi ya 1000 kwenye mechi hii pale Meridianbet.
Unaambiwa tangu Chelsea washinde fainali ya UEFA Champions League Final mwaka 2021 dhidi ya Manchester City imekuwa ngumu kwao kupata ushindi dhidi ya vijana hawa wa Pep Guardiola wakijitahidi sana ni sare.