Kuna mechi ambazo huwa tu mechi, na kuna mechi ambazo huandika historia kabla hata hazijaanza. Ile ya leo kati ya France na Spain, itakayoanza saa 22:00 usiku. Ni nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Dunia 2026, na wengi tayari wanaiita “fainali kabla ya fainali.”
Sababu ni rahisi hizi ndizo timu mbili zilizoingia kwenye mashindano huku zikiwa vipenzi na kupewa nafasi kubwa ya kutwaa taji, na zote mbili zimethibitisha hilo uwanjani. France wamefika hapa bila kupoteza hata mechi moja sita kati ya sita huku wakiongozwa na Kylian Mbappé, ambaye tayari amevunja rekodi kwa kufunga mabao nane kwenye makombe mawili ya dunia mfululizo.
Spain nao, ingawa safari yao imekuwa na mikwaruzo zaidi mabao ya ushindi yakija dakika za mwisho mara kadhaa wameonyesha nidhamu ya hali ya juu ulinzini, wakiwa hawajafungwa bao kwa mechi sita mfululizo kabla ya mchezo wao dhidi ya Belgium.
Lakini zaidi ya matokeo na takwimu, kuna hadithi ya kibinadamu inayowavuta mashabiki Kylian Mbappé na Lamine Yamal, wapinzani wa Real Madrid na Barcelona, sasa wanavaa jezi za nchi zao wakikutana kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka duniani kwa mara ya kwanza.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Wamekutana mara kumi huko nyuma kwenye Ligi na Kombe za Uhispania na Yamal ndiye mwenye rekodi bora zaidi ya ushindi, lakini ni Mbappé aliyefunga mabao mengi zaidi kati yao. Historia yao ya kitaifa inamuunga mkono Yamal, ambaye alikuwa shujaa wa Spain walipoifunga France 2-1 kwenye nusu fainali ya Euro 2024.
Vitani mle uwanjani, mechi hii itakuwa mapambano ya falsafa mbili tofauti za soka. Spain, chini ya Luis de la Fuente, wanapenda kumiliki mpira na kuutumia kuvunja mistari ya wapinzani polepole silaha yao kuu ikiwa ni Rodri na Pedri katikati ya uwanja.
France, chini ya Didier Deschamps, wamejengwa kucheza bila mpira mwingi na kushambulia kwa kasi ya umeme mara wanapouchukua, wakitegemea mchanganyiko wa Mbappé, Dembélé na Olise. Hali ya kiafya ya Aurélien Tchouaméni bado ni jambo la kutazamwa kwa karibu na kambi ya Ufaransa. Yeyote atakayeshinda, atapanda hatua moja karibu na taji la dunia, akisubiri mshindi wa Argentina dhidi ya England kwenye fainali ya Julai 19.