JKT Tanzania vs Yanga SC ni leo Mei 16, 2026 hatua ya robo fainali kwa wababe wawili kusaka tiketi kutinga hatua ya nusu fainali.
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo saa 12:30 jioni mshindi atakata tiketi moja kwa moja hatua inayofuata na atakayepoteza mwendo atakuwa amemaliza mpaka wakati ujao 2027.
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Abdihamid Moalin amesema kuwa wamefanya maandalizi mazuri kwa mchezo wa hatua ya robo fainali na malengo ni kusonga mbele hatua inayofuata.
Ikumbukwe kwamba ni vita ya mabingwa watetezi dhidi ya timu iliyofungwa kwenye hatua ya nusu fainali 2025 leo katika kambi za jeshi.
Kocha huyo amesema: “Tunatambua mchezo utakuwa mgumu tumefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo na malengo ni kuona kwamba tunasonga mbele hatua inayofuata,”.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.