Mwanariadha nyota wa Tanzania, Alphonce Simbu ametwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Kiume wa Mwaka katika Tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) 2025.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam.
Tuzo za BMT zimeendelea kuwa jukwaa muhimu la kutambua na kuthamini mafanikio ya wanamichezo, makocha na wadau wa michezo waliotimiza viwango bora ndani na nje ya nchi kwa mwaka 2025.
