Tabata Kisukuru Yapata Tabasamu Baada ya Msaada wa Meridianbet

Kama kawaida ilivyo kwa wakali wa ubashiri Meridianbet kurejesha kwa jamii imekuwa ni kawaida yao na leo hii ilikuwa ni zamu ya taasisi ya The Community Centre for Preventive Medicine iliyopo Tabata Kisukuru

Msafara huo wa kufika katika taasisi  hiyo ambayo inapatikana maeneo ya Tabata Kisukuru uliongozwa na Afisa Mahusiano Nancy Ingram akiwa na wenzake ambao kwa pamoja walipokelewa vyema kabisa na uongozi wa Taasisi hiyo.

Bila kupoteza muda kabisa wawakilishi hao wa Meridianbet Kampuni kubwa ya ubashiri Tanzania walianza kufanya kilichowapeleka ambacho kilikuwa ni kutoa vyakula na vifaa vya usafi binafsi ambavyo waliviandaa kwaaajili ya kutoa msaada kwenye Taasisi hiyo wanayoishi wazee au watu wasiojiweza.

Vyakula hivyo ni kama vile mchele, sukari, mafuta ya kupikia sabuni, pamoja na vifaa vya usafi wa mwili kwani usafi katika maeneo hayo ni muhimu sana kutokana na wingi wa watu ambao wanaishia  huko.

Kampuni inalenga kushirikiana na taasisi hiyo katika kuhakikisha wazee hao wanapata mlo kamili ili waweze kupata nguvu lakini pia kuhakikisha wanatumia sabuni kwenye usafi wao binafasi ili wajilinde na magonjwa mbalimbali mbayo yanatokana na uchafu.

Utajiri wako upo kwenye michezo ya Kasino siku ya leo ingia na ucheze Poker, Keno, Roulette, Aviator, Superheli  na ukusanye maokoto zaidi na zaidi. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz kubashiri mechi zote.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Afisa Mahusiano wa Kampuni hiyo Nancy Ingram alisema kuwa, “Tunatambua mchango mkubwa wa wazee katika jamii yetu, na ni jukumu letu kuhakikisha wanapata faraja na msaada wanapouhitaji. Hii ni sehemu ya dhamira yetu ya kuendelea kusaidia jamii,”

Na pia kwa upande wa Taasisi hiyo huko Tabata Kisukuru  baada ya kupokea vyakula hivyo na vifaa vya usafi walisema kuwa, “Tunafurahi kuona Meridianbet imetambua changamoto yetu ya uhaba vya vyakula na vifaa vya usafi  na kuja na suluhisho.  Msaada huu ni sehemu ya juhudi za kuimarisha huduma za jamii Dar es Salaam na kusaidia makundi maalum kama wazee.”

Kwa msaada huo ambao Meridianbet ilipeleka kwa wazee hao, inathibitisha kuwa kampuni hiyo si kwaajili ya michezo tuu bali ni kwaajili ya kuangalia na kutatua changamoto ambazo zinaikabili jamii yetu kwenye sekta mbalimbali ikiwemo na afya pia.

Kampuni hiyo itaendelea siku zote kuwaunga mkono watu wenye uhitaji katika jamii yetu kwani wao na jamii wanategemeana kwa kila kitu. Lakini pia Kampuni hiyo inawashihi watu kutunza mazingira kwa kutokutupa taka hovyo ili kujiepusha na magonjwa mbalimbali.