Simba SC 1-0 Mafunzo FC ni matokeo rasmi mchezo wa hatua ya robo fainali Muungano Cup 2026.
Goli la Simba SC limefungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 54. Mchezaji huyo alianzia benchi amekuwa ni super sub.
Katika dakika 45 za mwanzo wababe hawa wawili walishuhudia ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex ukisoma Simba SC 0-0.
Mshindi wa mchezo wa leo Aprili 23, 2026 anakwenda kumenyana na Mlandege katika hatua ya nusu fainali ya pili.
Mshindi wa mchezo wa fainali ya kwanza Yanga SC vs Azam FC atakutana na mshindi wa nusu fainali ya pili katika mchezo wa hatua ya fainali.
Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa taji hili ni Yanga SC ambao walianza kukata tiketi kwenye mchezo wa ufunguzi Aprili 21, 2026 wakiichapa Muembe Makuti magoli 4-0.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.