Singida Black Stars mpaka wakati ujao

BAADA ya kufungashiwa virago kwenye hatua ya robo fainali Muungano Cup 2026, Singida Black Stars wanarejea nyumbani kwa maandalizi ya mechi zijazo.

Timu hiyo ilipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa magoli 2-1 dhidi ya Mlandege ambao wametinga hatua ya nusu fainali.

Timu hiyo ilianza kupata goli dakika ya 9 kupitia kwa Daud halikudumu mpaa mwisho wa mchezo mara baada ya Mlandege kupindua meza kupitia kwa Samatta na Mbappe wa Zanzibar.

Mapema Aprili 24, 2026 Singida Black Stars wameanza safari kurejea Singida kwa maandalizi ya mechi zijazo ndani ya NBC Premier League.

Timu tatu kutoka ligi ya NBC zimesonga hatua inayofuata ambapo Yanga SC vs Azam FC na Simba SC ambayo itamenyana na Mlandege ya Zanzibar.

Mabingwa watetezi ni Yanga SC ambao wanatarajiwa kushuka uwanjani kesho Aprili 25, 2026 kumenyana na Azam FC hatua ya nusu fainali ya kwanza.

Mshindi wa nusu fainali ya kwanza atamenyana na mshindi wa nusu fainali ya pili kwenye mchezo wa fainali.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.