Kombe la Shirikisho la CRDB Laendelea Kutimua Vumbi Leo

Michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB (CRDB Bank Federation Cup) inaendelea kutimua vumbi leo kwa mechi mbili ambapo Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc watakuwa wenyeji wa Greenland FC katika dimba la Meja Janerali Isamuhyo majira ya saa 1:00 usiku.

Mapema saa 10:00 jioni Wakusanya ushuru wa Jiji la Dar, KMC FC watakuwa wenyeji wa Bandari Tanzania katika dimba la KMC Complex.

16:00 KMC FC Vs Bandari Tanzania
🏟️ KMC Complex

1:00 Simba SC Vs Greenland FC
🏟️ Meja Janerali Isamuhyo