Yanga wamekamilisha usajili wa kiungo wa Vipers, Allan Okello (25) kwa mkataba wa miaka miwili na nusu✅
Haikuwa kazi nyepesi kwani wiki hii vilabu vya MC Alger na Al Ahli Tripoli ya Libya,vilituma ofa nono ili kumpata kijana.
Baada ya Rais wa Yanga kupata hizo taarifa akapanda ndege chapu kuelekea Uganda ili kumalizana na Rais wa Vipers,Lawrence Mulindwa.
Bado mazungumzo yalikuwa magumu ila Eng. Heris,ameshinda vita na Okello ni balaa jipya Tanzania.
Muda huu Heris anaelekea Airport ili kuchukua ndege ya Tanzania,kwani biashara ya Okello imefungwa rasmi✅
