SIMBA SC imepishana na kombe la kwanza ndani ya 2026 baada ya kupoteza nusu fainali ya kwanza mbele ya Azam FC.
Januari 8 2026 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 1-0 Simba SC bao la ushindi likifungwa na Lameck Lawi dakika ya 73.
Hili ni taji la kwanza ndani ya 2026 Simba SC inapishana nalo mazima ambapo tayari Azam FC imetinga hatua ya fainali inamsubiri mshindi wa mchezo wa leo.
Mshindi wa mchezo kati ya Yanga SC vs Singida Black Stars yataamua nani atakayecheza na Azam FC kwenye hatua ya fainali.
Mfungaji wa bao la ushindi kwenye mchezo huo Lameck Lawi alichaguliwa kuwa mchezaji bora na alizawaidwa kiasi cha milioni mbili.
Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker kwenye mechi tatu ambazo ameongoza kikosi hicho ushindi ni mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.