Nyota wa Ghana, Semenyo, Asajiliwa Manchester City

Klabu ya Manchester City imetangaza kumsajili winga Antoine Semenyo kwa ada ya pauni milioni 62.5 (Euro milioni 72) kutoka klabu ya AFC Bournemouth.

Semenyo 26, raia wa Ghana amesaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo mpaka Juni 2031 na atavaa jezi namba 42 iliyowahi kuvaliwa na nyota wa zamani wa Man City na Ivory Coast. Bournemouth inatarajiwa kunufaika na asilimia 10 za mauzo ya siku za usoni.

Nyota huyo wa zamani wa Bristol City anakuwa mchezaji aliyeuzwa ghali zaidi kwenye historia ya klabu hiyo ambayo pia inatarajiwa kupokea pauni milioni 1.5 kutokana utendaji wa nyota huyo huko Man City.