KOCHA WA YANGA ATOA TAMKO DHIDI YA AZAM KESHO!

“Hatuna muda wa kutosha wa kujiandaa na mchezo, lakini tupo tayari kushindana na Azam FC. Utakuwa ni mchezo wenye msisimko wa aina yake kwangu na kwa kocha wa Azam kwani namfahamiana nae kwa miaka 25, utakuwa wasaa mzuri kati yetu.“

“Naheshimu kila timu, Azam wana timu nzuri, wana kocha mzuri. Tutajitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu. Ni matarajio yangu tutacheza mchezo mzuri kuliko michezo iliyopita. Kila mchezo ni tofauti, na kila mpinzani ni tofauti. Kuna muda itabidi tubadilishe mfumo na tutafuta njia na mfumo sahihi wa kupata matokeo dhidi ya Azam”

“Kwenye maisha hupaswi kujiwekea matarajio asilimia mia moja, lolote linaweza kutokea, hiyo ndio tabia ya mpira wa miguu. Ni kweli tunaweza kukosa wachezaji wengi. Nafahamu Azam wamepata zaidi ya siku saba mpaka nane za kujiandaa. Tumeshacheza michezo miwili wakati wao wakiwa wamepumzika. Lakini nashukuru nimebarikiwa kuwa na wachezaji wazuri sana”