AUCHO KUIKOSA AZAM FC

KIUNGO wa Yanga, chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi atakosekana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Novemba 2 2024.

Ni NBC wadhamini wa ligi yenye ushindani mkubwa huku Azam TV kwenye upande wa kurusha mubashara mechi zote za ligi msimu wa 2024/25.

Sababu kubwa ya Aucho kukosa mchezo wa kesho ni kadi tatu za njano ambazo alizipata kwenye mechi tofauti za ligi uwanjani.

Rekodi zinaonyesha kuwa kadi ya kwanza ilikuwa Septemba 29 2024 dakika ya 63 dhidi ya KMC, kadi ya pili Oktoba 19 2024 dhidi ya Simba dakika ya 78 na kadi ya tatu ilikuwa Oktoba 30 dakika ya 26 dhidi ya Singida Black Stars.

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga kuelekea mchezo huo amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa na ugumu kutokana na kucheza mechi mbili mfululizo huku Azam FC ikiwa haijacheza lakini watapambana.

“Huwezi kulinganisha mechi na ukizingatia kwamba tumetoka kucheza mechi mbili hivi karibuni huku wapinzani wetu Azam FC wakiwa wamepumzika kwa muda wa siku 7, lakini tupo tayari kwa kuwa tuna wachezaji wazuri.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.