Leo Septemba 29, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakuwa ugenini ikimenyana na Madagascar, mechi ya kufuzu AFCON 2027 saa 11 jioni, Meknes, Morocco.
Huu ni mchezo wa pili kwa Kundi L ambapo kete ya kwanza ikiwa nyumbani Tanzania ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 Guinea Bissau inayoongoza kundi ikiwa na pointi 3 kibindoni.
Tanzania inaburuza mkia ikiwa haina pointi inakutana na timu iliyo nafasi ya 3 na haijakusanya pointi pia ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Nigeria.
Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Taifa Stars amesema wanatambua mchezo utakuwa mgumu wapo tayari kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa hatua ya makundi.
“Tunatambua mchezo utakuwa mgumu, tupo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi kikubwa nikuona kwamba tunacheza vizuri tukiwa ugenini,”.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.
Soccer Football - International Friendly - Italy v Turkey - Stadio Renato Dall'Ara, Bologna, Italy - June 4, 2024 Turkey's Abdulkadir Omur shakes hands with Italy's Riccardo Calafiori after the match REUTERS/Daniele Mascolo