Home Sports YANGA WABABE KARIAKOO DABI

YANGA WABABE KARIAKOO DABI

MSIMU wa 2023/24 kwa watani wa jadi Yanga na Simba umegota mwisho huku Yanga wakiwa ni wababe ndani ya ligi nje ndani.

Aprili 20 2024 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Yanga 2-1 Simba na ule mchezo wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba 1-5 Yanga.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza ulichezwa Novemba 5 2023 Yanga walikomba pointi tatu mazima na leo wamekomba pointi tatu mazima.

Kwenye msako wa pointi sita, Simba wameambulia patupu na Yanga wamesepa nazo zote mazima wakiwa ni wababe wa Kariakoo Dabi.

Yanga inafikisha pointi 58 ikiwa inanukia kuutwaa ubingwa wa ligi kwa mara nyingine tena kwa kuwa mchezo ambao ulikuwa mgumu kwao ni huu wa leo dhidi ya Simba.

Previous articleF T: YANGA 2-1 SIMBA
Next articleMAOKOTO NA BONASI ZA KASINO UNAZIPATA UKISHIRIKI SHINDANO LA EXPANSE