Home Uncategorized SIMBA HAIJAPOTEZA MATUMAINI

SIMBA HAIJAPOTEZA MATUMAINI

UONGOZI wa Simba licha ya Machi 29 2024 mambo kuwa magumu kwao kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-1 Al Ahlyumebainisha kuwa matumaini bado yapo kufanikisha malengo yao.

Ipo wazi kwamba malengo ya Simba kwenye anga la kimataifa ni kufika hatua ya nusu fainali jambo ambalo wanalipambania kwa sasa.

Katika mchezo huo Simba ilifungwa bao la mapema dakika ya tano lilidumu mpaka dakika ya 90 na ziliongezwa dakika tano kwa timu zote mbili.

Mfungaji wa bao pekee la ushindi kwa Al Ahly ni Ahmed Kouka ambaye alitumia makosa ya safu ya ulinzi wa Simba kupata bao hilo la mapema ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua kwamba walikuwa wanahitaji ushindi lakini haikuwa bahati kwao na mwisho wakapoteza mchezo huo lakini bado wapo imara.

“Tulikuwa bora kwenye mchezo lakini bahati haikuwa upande wetu nafasi ambazo tulizipata tulizokosa kwenye mchezo hivyo hakuna namna tutafanyia kazi makosa ili kufanya vizuri kwa mechi zijazo kikubwa mashabiki tuendelee kuwa pamoja,”.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Misri Aprili 5 ambapo mshindi wa jumla atajulikana kwenye mchezo huo.

Previous articleYANGA: WANAOFIKIRI MWISHO WETU UMEFIKA HAWATAAMINI
Next articleAL AHLY WAMEACHA BALAA SIMBA, TAMKO LATOLEWA