Home Sports YANGA: WANAOFIKIRI MWISHO WETU UMEFIKA HAWATAAMINI

YANGA: WANAOFIKIRI MWISHO WETU UMEFIKA HAWATAAMINI

ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wale wengi wanaofikiria safari ya Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika itagotea hatua ya robo fainali hawataamini macho yao kwa kuwa wanaamini watafanya vizuri.

Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, Machi 30 inatarajiwa kutupa kete ya kwanza katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrik Kusini.

Kamwe amebainisha kuwa anasikia wengi wanasema kwamba hawana ubavu wa kupambana na wapinzani wao jambo ambalo sio kweli kwa kuwa wanawachezaji wenye uwezo mkubwa uwanjani katika kutimiza majukumu yao.

“Wale ambao wanasema kwamba safari yetu itakuwa ngumu, wasubiri na waone namna ambavyo tutawafanya wapinzani wetu Mamelodi Sundowns inabidi wakumbuke kwamba tunaanza kazi nyumbani hakuna jambo dogo kwetu lazima tufanye kweli.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu hilo halipingiki lakini kusema kwamba tunawahofia kwa kuwa wanatoka Afrika Kusini hapana Yanga tumeshavuka hatua hizo sasa tunakwenda kupambana kwa ajili ya maslahi ya taifa tunaamini tutafanya vizuri,”.

Previous articleMERIDIANBET YAGAWA REFLECTORS KWA BODABODA
Next articleSIMBA HAIJAPOTEZA MATUMAINI