LIGI Kuu Bara F2 2024 inarejea kwa mara nyingine tena baada ya mapumziko yaliyotokana na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, (AFCON).
Ni hatua ya makundi Stars iligotea ikukusanya pointi mbili katika michezo mitatu iliyocheza huku bao likifungwa moja na nyota Simon Msuva.
Leo Kagera Sugar yenye kocha mpya Felix Minziro ambaye alianza msimu akiwa ndani ya Tanzania Prisons inakibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Yanga inayofundishwa na Miguel Gamondi.
Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Marwa Chamberi ameweka wazi kuwa wanatambua kuwa walipoteza mchezo wao uliopita hivyo makosa wameyafanyia kazi.
“Kwenye kipindi hiki cha AFCON kuna makosa ambayo tulifanyia kazi kwa ajili ya mechi zetu kuelekea mchezo wetu dhidi ya Yanga tunaamini kwamba tutafanya vizuri.
“Kikubwa ni kwamba tulipata muda mzuri wa maandalizi tumetumia vizuri kipindi hiki kwa ajili ya kuona kwamba tunakuwa imara, hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.
Kagera Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 13, Yanga nafasi ya pili ina pointi 30.